Simba Sc yaitesa Mbabane Swallows, yaichapa 4-0 nyumbani kwao

|
Meddie Kagere akishangilia baada ya kuifungia Simba bao la nne.

Wekundu wa Msimbazi Simba SC (wenye mashindano yao) imeiangushia dozi nene ya kipigo cha mabao 4-0 timu ya Mbabane Swallows ya eSwatin katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa kwenye Dimba la Mavuso nchini humo.

Simba iliyokuwa ugenini imejipatia mabao yake kupitia kwa Clatous Chama aliyefunga mabao mawili dakika ya 28 na 33, huku mengine yakifungwa Emmanuel Okwi dakika ya 52 na Meddie Kagere dakika ya 63.

Ushindi huo unaifanya Simba kufuzu hatua hiyo na kuingia hatua ya kwanza kwa jumla ya mabao 8-1 kufuatia ushindi wa mabao 4-1 iliyoupata katika mchezo wa kwanza uliopigwa wiki moja iliyopita Jijini Dar es Salaam.

Simba sasa inasubiri mshindi kati ya Nkana Red ya Zambia na UD Songo ya Msumbiji.

CAF
Maoni