Simba yaigonga Al Ahly 1-0 Ligi ya Mabingwa Afrika

|
Beki wa Simba Pascal Wawa alipokuwa akiteta jambo la Junior Ajayi wakati mpira ukiendelea.

Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Bao pekee la Simba limefungwa na Meddie Kagere dakika ya 65 akimalizia pasi ya kichwa kutoka kwa Nahodha John Bocco baada ya majaro ya Zana Coulibali kutoka winga ya kulia.

Matokeo hayo yameifanya Simba kufikisha pointi sita kwenye kundi lake la D ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Al Ahly ambao wana pointi saba.

Wapinzani wengine wa Simba kwenye kundi hilo AS Vita na JS Saoura wanakutana usiku wa leo katika mchezo utakaopigwa nchini Algeria saa 4:00 usiku LIVE #ZBC2

Baada ya mechi za leo, mechi zinazofuata zitapigwa Machi 9, mwaka huu ambapo Simba itawafuata JS Saoura nchini Algeria huku AS Vita ikiwakaribisha Al Ahly nchini DRC.

CAF
Maoni