Solari athibitishwa kuwa kocha mkuu Real Madrid

|
Santiago Solari ambaye sasa amekuwa kocha mkuu wa Real Madrid.

Klabu ya Real Madrid imemthibitisha Santiago Solari kuwa kocha mkuu wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu hadi Juni 2021. .

Solari alikuwa anakaimu nafasi hiyo baada ya alyekuwa kocha mkuu kutimuliwa kutokana na mwenendo mbaya wa timu msimu huu ikiwepo kipigo cha 5-1 ilichokipata kwenye El Clasico kutoka kwa Barcelona Oktoba 28, 2018. .

Tangu akabidhiwe timu, Solari ameiongoza kwenye michezo minne na kushinda yote huku ikifunga mabao 15 na kuruhusu mabao mawili pekee.

Soka
Maoni