Tanzania yafuzu AFCON baada ya miaka 39

|
Mechi ilikuwa LIVE ZBC 2.

Tanzania imefuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2019 zitakazofanyika nchini Misri mwezi Juni mwaka huu (AFCON 2019) ikiwa ni mara ya pili kwa Tanzania kufuzu fainali hizo ikiwa imefanya hivyo pia mwaka 1980.

Hatua hiyo ni baada ya kuichapa Uganda mabao 3-0 na kushika nafasi ya pili kwenye kundi L, ikifikisha pointi 8 nyuma ya vinara Uganda wenye pointi 13. 

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es salaam, mabao ya Tanzania yamefungwa na Saimon Msuva dakika ya 21 akimalizia pasi ya John Bocco, Erasto Nyoni kwa penati baada ya beki wa Uganda kuunawa mpira wa Mbwana Samatta ndani ya eneo la hatari dakika ya 51 na bao la tatu likifungwa na Agrey Moris kwa kichwa akimalizia pasi ya John Bocco dakika ya 57. 

FT: Tanzania 3-0 Uganda

FT: Cape Verde 0-0 Lesotho

CAF
Maoni