Tanzania yajinadi kudhibiti uingizwaji dawa za kulevya

|
Dawa za kulevya zikiwa zimekamatwa na Kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa hizo (Maktaba)

Kamishna wa Mamlaka wa Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania, Roger Siyanga amesema kiasi cha uingizwaji wa dawa hizo nchini kimepungua lakini bado tatizo hilo halijamalizika kutokana na kwa sasa wasafirishaji wakubwa wa dawa hizo wamebadili mtindo wa kuingiza bidhaa hiyo.

Kamishna Siyanga amesema, waigizaji hao wakubwa kwa sasa wanaingiza kiwango kidogo cha kuanzia kilo nne hadi tano licha ya takwimu za mwaka 2018 kuonesha kuwa tani 9000 zilikamatwa kupitia njia za majini na tani 1000 kupitia nchi kavu.

Kamishna wa mamlaka hiyo pia amebainisha mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salam kuwa wamekuwa na ushirikiano na mamlaka nyingine katika kufanikisha udhibiti wa uingizaji wa dawa za kulevya nchini, ushirikiano uliofanikisha kwa kiwango kikubwa kupunguza uingizaji na utumiaji hadharani.

Siyanga amesema, Mamlaka hiyo kwa sasa ipo kwenye mkakati wa kupata takwimu sahihi za watumiaji wa dawa za kulevya na wanatarajia kupitia maadhimisho ya miaka miwili ya mamlaka hiyo inayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu kushirikiana na taasisi hizo katika kuimarisha mapambano dhidi ya dawa hizo

Biashara
Maoni