Tanzania yawekwa chungu cha nne kuelekea makundi ya AFCON 2019

|
Vyungu hivyo vimepangwa kulingana na viwango vya soka vya CAF.

Droo ya upangaji wa makundi ya fainali za (AFCON 2019) inatarajiwa kufanyika Aprili 12 mwaka huu nchini Misri ambapo Tanzania imewekwa kwenye chungu cha nne ikiwa pamoja na mataifa ya Mauritania, Namibia, Kenya, Benin na Madagascar.

Vyungu hivyo vimepangwa kwa mujibu wa viwango vya soka vya CAF, ambapo makundi sita yanatarajiwa kuundwa, kila kundi likiwa na timu nne na timu zilizo kwenye chungu kimoja hazitakutana kwenye kundi moja.

Kati ya mataifa 24 yaliyofuzu fainali hizo, ni mataifa matatu ambayo yamefuzu kwa mara ya kwanza katika historia yake ambayo ni Burundi, Mauritania na Madagascar

Hii ni mara ya kwanza kwa Afrika Mashariki kuingiza timu nne kwa wakati mmoja kwenye michuano hiyo, ambazo ni Tanzania, Uganda, Kenya na Burundi.

CAF
Maoni