TPL: Azam yabanwa Iringa, Coastal ikitamba Mwanza

|
Lipuli FC vs Azam FC.

Azam FC imetoka sare ya bao 1-1 ikiwa ugenini dhidi ya Lipuli FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Lipuli FC ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 45 kupitia kwa Daruesh Saliboko kabla ya Azam FC kujipanga na kusawazisha bao hilo dakika ya 81 kupitia kwa Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Matokeo hayo yameifanya Lipuli ifikishe pointi 37 na kupanda hadi nafasi ya tatu huku Azam FC walio nafasi ya pili wakifikisha pointi 49 nyuma ya vinara Yanga wenye pointi 58.

Kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Coastal Union imefanikiwa kuchukua pointi tatu ugenini kwa kuichapa Mbao FC bao 1-0.

Licha ya Mbao kumiliki zaidi mpira na kufanya mashambulizi mengi langoni kwa Coastal, nafasi pekee aliyoipata Raizin Hafidh dakika ya 60 aliitumia na kuipatia Coastal bao pekee lililoipa alama tatu ugenini.

 Matokeo ya mechi zote za leo yako hivi:  

FT: African Lyon 0-0 Ruvu shooting.

FT: Mbao FC 0-1 Coastal Union (Raizin Hafidh 60’).

FT: TZ Prisons 1-0 Stand United (Adam Adam 51’).

FT: Mwadui FC 1-0 Mtibwa Sugar (Salim Aiyee 75’).

FT: Lipuli FC 1-1 Azam FC (Daruesh Saliboko 45’: Salum Abubakar 81’).

FT: Ndanda SC 2-0 Kagera Sugar (Yusuf Mhilu 40’, Mohamed Mkopi 64’).

 

TPL
Maoni