Trump amtimua mwanasheria mkuu wa Marekani

|
Aliyekuwa Mwanasheria mkuu wa Marekani, Jeff Sessions aliyefukuzwa na Rais Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump amemfukuza kazi Mwanasheria mkuu wa nchi hiyo Jeff Session.

Akitoa taarifa kupitia mtandao wa Twitter, Rais Trump amesema nafasi yake itashikwa kwa muda na mwanasheria Matthew Whittaker.

Katika ukurasa wake rasmi wa Twitter Rais Trump amemshukuru Jeff Sessions kwa kazi yake hiyo na kumtakia kila la kheri.

Kwa upande wake, Jeff Sessions katika barua yake ya kujiuzulu, aliweka bayana kuwa uamuzi wa kuondoka katika nafasi hiyo haukuwa wake.

Katika barua isiyokuwa na tarehe alimjulisha Rais Trump kwamba anawasilisha barua yake ya kujiuzulu kama alivyomtaka afanye hivyo.

Utawala
Maoni