Trump atofautiana na wenzake G7

|
Rais Trump na viongozi wenza wa Ujerumani, Angela Markle na Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May

Mazungumzo katika mkutano wa mataifa yaliyoendelea kiviwanda dunia (G7) yanayofanyika nchini Canada yameshindwa kutatua tofauti kubwa zilizopo kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na viongozi wa mataifa mengine wanachama.

Tofauti hizo zilizuka hadharani siku ya Ijumaa hususan kuhusu biashara.

Washirika wa Marekani wamekasirishwa na hatua ya Rais Trump ya hivi karibuni kutoza ushuru vyuma na bidhaa za Aluminium, hatua inayozua hofu ya kuzuka kwa vita vya kibishara.

Mjini Quebec, mkutano huo ulianza vibaya na umemalizika bila makubaliano hayo ya pamoja.

Tofauti kati ya Trump na viongozi wengine sita zinatokana na masuala ya kibiashara  zinashirikisha hali ya tabia nchi, uhusiano na Iran na mgogoro kati ya Israel na Palestina.

Utawala
Maoni