Trump na mkewe watoa heshima za mwisho wa Bush HW

|
Rais wa Marekani, Donald Trump na mkewe Melania, wakitoa heshima za mwisho kwenye jeneza la aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo 1989 -1993

Rais wa Marekani, Donald Trump na mkewe Melania walikuwa ni miongoni mwa waliotoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo wa 41, George HW Bush wakati wa kuaga kitaifa katika eneo muhimu la nchi hiyo la Capitol, Washington.

Trump na mkewe walifaikiwa kufika kwenye eneo la tukio hilo maarufu rotunda kwa muda mfupi ambapo pia wananchi wengine waliruhusiwa kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kufanyika kwa mazishi, kesho Jumatano.

Licha ya Trump kuwa katika mgogoro na familia ya Bush mara kadhaa lakini imedhibitishwa kuwa atahudhuria ibada ya mazishi kesho.

Marehemu Bush, ambaye alifariki Ijumaa iliyopita akiwa na miaka 94, anataraji kuzikwa baadaye nyumbani kwake Texas karibu na kaburi la mkewe, Barbara aliyefariki miezi saba iliyopita.

Jeneza lake mapema kabla ya kuondolewa huko Texas lilipigiwa mizinga 21 na saluti kama heshima na kisha kubebwa kwa Ndege maalum ya Air Force One hadi Washington kama heshima kwa kiongozi huyo aliyeiongoza Marekani kwa vipindi viwili.

Marehemu Bush, alihudumu kama Rais wa nchi hiyo wa 41, kati ya 1989  na 1993 na alikuwa katika matibabu tangu Aprili akisumbuliwa na maradhi ya maumbukizi kwenye damu.

Maisha
Maoni