Twiga Stars yawatoa hofu Watanzania kuelekea mchezo dhidi ya DRC

|
Twiga Stars wanaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa JMK Youth Park, Kidongo Chekundu.

Timu ya taifa ya Tanzania ya wanawake Twiga Stars, wamewataoa hofu Watanzania kuelekea kwenye mchezo wao wa April 5, mwaka huu dhidi ya DR.Congo ikiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu Olimpiki,mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kocha Msaidizi wa Twiga Stars, Edna Lema amesema kikosi chake kipo katika mazoezi makali kuelekea mchezo huo utakaochezwa wiki ijayo na marudiano yake yatafanyika Aprili 9 mwaka huu huko DR Congo.

Soka la wanawake
Maoni