Uchaguzi DRC: Utangazaji matokeo wasogezwa mbele zaidi

|
Rais wa Tume ya Uchaguzi DRC (CENI) akitangaza kuahirishwa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita akitaka kupokelewa kwa chini ya asilimia 50 ya matokeo yote na tume yake.

Tume ya uchaguzi nhini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imetangaza kuwa matokeo ya uchaguzi mkuu hayatatoka Jumapili kama ilivyopangwa awali kutokana na kuchelewa kwa matokeo mengi kutoka vituoni huku CENI ikisema imepokea asilimia 47 ya karatasi za matokeo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Al Jazeera Rais wa tume hiyo, Corneille Nangaa ametangaza hivyo Jumamosi.

Matokeo ya awali ya uchaguzi huo yalitarajiwa kutangazwa siku ya Jumapili huku Marekani ikipeleka wanajeshi wake 80 nchini Gabon ikiwa ni hatua ya tahadhari ya kusaidia kulinda amani nchini DRC iwapo kutatokea vurugu zinazohusiana na uchaguzi huo.

Hatua hiyo ya CENI imezua hofu ya kufanyika kwa wizi wa kura huku wachambuzi wa siasa za nchi hiyo wakidai kucheleweshwa zaidi kutangazwa kwa matokeo hayo kunaweza kukapelekea kuzuka kwa machafuko kama ilivyotokea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kwenye uchaguzi wa mwaka 2006 na 2011.

Bado haijafahamika siku rasmi ambayo matokeo hayo yatatangazwa huku rais wa CENI akinukuliwa akisema “Haitawezekana kutangaza matokeo siku ya kesho (Jumapili)”

Nangaa alisema kuchelewa huko kunatokana na ukubwa wa nchi hiyo pamoja na changamoto za vifaa na njia.

Maisha
Maoni