Uchunguzi wa mwanafunzi wa UDSM kutekwa wawekwa wazi

|
Kamanda wa Kanda Maalum, Lazaro Mambosasa akizungumza na vyombo vya habari

Polisi Kanda maalumu ya Dar Es Salaam imethibitisha kuwa madai ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Abdul Nondo kuwa alitekwa si ya kweli bali alitoa taarifa hizo kwa maslahi binafsi ikiwa ni pamoja na kujitafutia umaarufu.

Kamanda  wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa  amewaambia waandishi wa habari kuwa baada ya jeshi la Polisi kusikia taarifa hizo, lilianza ufuatiliaji ili kubaini ukweli wa tukio hilo ikiwa ni pamoja na kufungua jadala la uchunguzi.

Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa, Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Machi 7,  mwaka huu lilipata taarifa  kutoka Iringa  kuwa mwanafunzi huyo ameonekana mkoani humo akiwa wilayani Mafinga.

Katika hatua nyingine Kamanda Mambosasa amebainisha hatua ambazo  zinachukuliwa dhidi ya Abdul Nondo mara baada ya kubainika kuwa hakutekwa ikiwa ni pamoja na kufungulia jalada kwa ajili kumpekeka mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Utawala
Maoni