UEFA kuja na mashindano mapya ya vilabu Ulaya

|
Chama cha Soka Barani Ulaya (UEFA).

Chama cha Soka Barani Ulaya (UEFA) kimesema kipo kwenye hatua za mwisho kuja na michuano mipya kwa ngazi ya vilabu barani humo, ambayo itakuwa ni michuano ya tatu kwa ukubwa baada ya UEFA Champions League na Europa League.  

Mkuu wa Chama cha Vilabu barani Ulaya (ECA) Andrea Agnelli ndiye aliyetoa taarifa hiyo kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho unaofanyika nchini Croatia, lakini hajaweka wazi mfumo wa mashindano hayo utakavyokuwa.

Agnelli ambaye amewahi kuwa kiongozi wa klabu ya Juventus, amesema mfumo uliopo sasa kwa mashindano ya vilabu, unatakiwa kufanywa uwe wa kisasa zaidi.

UEFA
Maoni