Uganda: 29 wafariki kwa kuzama Ziwa Victoria wakitokea kwenye sherehe

|
Boti ndogo za wavuvi zimetajwa kuwa za kwanza kutoa msaada baada ya kutokea kwa ajali hiyo huku idadi kamili ya waliokuwemo kwenye boti iliyozama ikiwa haijulikani.

Watu 29 wamethibitishwa kufariki dunia nchini Uganda baada ya boti ndogo waliyokuwa wakisafiria kuzama kwenye Ziwa Victoria siku ya Jumamosi karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala.

Kwa mujibu wa jeshi la Polisi la Uganda watu hao ni sehemu ya watu wanaokabiliwa kufikia 100 waliokuwa wamepanda boti hiyo wakitokea kwenye sherehe.

Kwa mujibu wa vyombo vvya habari vya Uganda ajali hiyo ilihusisha pia watu wengine maarufu nchini humo akiwemo mdogo wa mfalme wa jadi wa tawala ya Buganda, Daudi Kintu Wasajja.

Ziwa Victoria limekuwa likihusika mara kwa mara kwenye ajali za majini huku lilikumbukwa kwa kuua zaidi ya watu 200 mwezi Septemba mwaka huu baada ya kivuko cha MV Nyerere cha Tanzania kuzama kwenye kisiwa cha Ukara.

Ajali ya jana [Jumamosi] imetokea kwenye wilaya ya Mukono iliyopo katika jiji la Kampala.

Msemaji msaidizi wa polisi, Patrick Onyango aliliambia shirika la utangazaji la Reuters: "Kwanza boti ilikuwa na watu wengi kupita kiasi na pili kulikuwa na hali mbaya ya hewa."

Tayari zaidi ya watu 20 wameokolewa kufuatia ajali hiyo huku idaidi ya watu ambao hawajulikani walipo ikiwa haijafahamika na jeshi la uokozi la Uganda linaendelea kufanya jitihada kuwatafuta.

Maisha
Maoni