Ujumbe wa R. Kelly kuhusu ziara yake ya muziki waamsha hasira

|
Mwanamuziki nyota wa Marekani, R. Kelly anayepingwa kila kona kutokana na kashfa ya madai ya kudhalilisha wanasichana kingono

Tangazo la mwanamuziki R Kelly la kuanza ziara ya maonesho ya muziki katika nchi za Australia, New Zealand na Sri Lanka, limekosolewa kila kona kutokana madai ya yanayomkabili mwanamuziki huyo kuhusu udhalilishaji wa kingono.

Mwanamuziki huyo nyota wa Marekani aliyevuma kwa mtindo wake wa muziki wa  R&B alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii ya Twitter, Facebook na Instagram kwa kuposti ratiba ya ziara yake hiyo ambayo hata hivyo baada ya hapo aliifuta.

Mpango huo wa ziara ya mwanamuziki huenda ukakumbana na vikwazo kufuatia Makala iliyoelezea madai ya kashfa ya ngono inayomuandama mwanamuziki huo kwa miongo kadhaa.

Wanasiasa wa ndani wametoa wito wa kuzuiwa kuingia nchini Australia.

Jana Jumanne, mshindi huyo wa tuzo ya Grammy mwenye miaka 52 alitwiti kwa kuandika "NEW TOUR ALERT", bila kutoa tarehe za matamasha hayo na wapi. Hata hivyo ujumbe huo ulipokelewa kwa hasira dhidi ya mwanamuziki huyo na wengi wa waliojibu walisema hakaribishwi kwenye nchi hizo.

Maisha
Maoni