Unataka kuishi maisha marefu,? Lala vizuri - Utafiti

|
Tafiti zinasema, iwapo mwanadamu atalala katika mazingira mazuri na kwa muda wa kutosha uwezekano wa kuishi muda mrefu ni wa lazima

Mtaalamu mmoja wa masuala ya Neva na Saikolojia amesema ili uweze kuishi maisha marefu ni lazima ukubaliane na hali ya kuwekeza katika kujipatia usingizi mzuri .

Profesa Matthew Walker wa Chuo Kikuu cha California , amesema "Usingizi ni kiungo muhimu cha kidemokrasia na mfumo wa afya ambao unapatikana bure.”

Wakati Profesa huyo akisema hvyo, jamii ya kisayansi nayo inaamini kwamba baada ya miaka 50, wataalamu wa usingizi kote duniani hawatafanya tafiti za kuangazia kile ambacho kinasababishwa na usingizi.

Sayansi imebaini kwamba ukosefu wa usingizi husababisha athari mbaya kwa miili na ubongo.

“Kila ugonjwa unaowauwa watu katika mataifa yaliyoendelea kama vile ugonjwa wa kusahau, saratani, magonjwa ya moyo, kunenepa kupita kiasi, kisukari, wasiwasi na hata mtu kutaka kujiua yanahusishwa na ukosefu wa usingizi.

Katika utafiti huo, wataalau hao wamesema, mifumo yote ya kisaikilojia katika mwili wa binadamu ama hata operesheni ya akili huimarishwa wakati mtu anapolala.

Utafiti huo umeongeza kuwa viungo hivyo vyote huathirika iwapo mtu anakosa usingizi mwanana na ni sharti usingizi huo uwe halisi ili viungo hivyo kuweza kuimarishwa.

Kwa wale wanaotimu sawa za kumfanya mtu apate usingizi zinahusishwa na kiwango cha juu cha hatari ya kupata saratani, maambukizi n ahata kupelekea vifo.

Maisha
Maoni