Usain Bolt kuanza majaribio ya soka Agosti 31

|
Usain Bolt akiwa kwenye mazoezi ya kusakata kabumbu.

Nyota wa mchezo wa riadha aliyeamua kuhamia katika soka Usain Bolt amekiri kuwa na hofu kuelekea mchezo wake wa kwanza wa majaribio akiwa na timu ya Central Coast Mariners inayocheza ligi kuu nchini Australia.

Mshindi huyo mara nane wa medali ya dhahabu ya Olympic katika mchezo wa riadha,  anaendelea kujifua kwa nguvu zote akiwa na Mariners na Agosti 31 atashuka dimbani kutupa karata yake ya kwanza kusaka tiketi ya kucheza soka la kulipwa.

Bolt anayeshika rekodi ya dunia kwenye mbio za mita 100 na 200 kiwango chake cha soka kimeimarika zaidi tangu ajiunge na timu hiyo kwa majaribio na kuna dalili ya kupewa mkataba rasmi wa kucheza soka la kulipwa klabuni hapo.

Michezo
Maoni