Waandamanaji waendelea kupinga rushwa mitaani Haiti

|
Wananchi wa Haiti wakiwa wamefurika mitaani kuipinga serikali yao wanayodaiwa imekidhiri kwa vitendo vya rushwa

Maelfu ya waandamanaji wameendelea kusalia katika mitaa ya mji mkuu wa Haiti wa Port-au-Prince huku wakikabiliana na Polisi wakipinga rushwa na hali ngumu ya kiuchumi nchini humo.

Waandamanaji wamefunga baadhi ya barabara kwa kuchoma matairi na kuteketeza magari kwa madai ya kuchoshwa na utawala mbovu wa kisiwa hicho kilichoko ukanda wa Caribbean na Pasific.

Mwishoni mwa wiki iliyopita mtu mmoja alikufa katika majibizano ya waandamanaji na polisi baada ya waandamanaji kushambulia kwa mawe nyumba ya Rais wa Haiti, Jovenel Moise.

Waandamanaji hao wamekuwa na hasira juu ya Mfumuko wa Bei wa Kiwango cha kupindukia unaozidi kuongezeka na kushindwa kwa Serikali kuchukua hatua dhidi ya ufisadi katika miradi ya mafuta nchini Haiti.

Tukio
Maoni