Wabunge Uingereza watoa karipio kali kwa Serikali

|
Bunge la Uingereza lililoionya Serikali

Wabunge nchini Uingereza wametoa karipio kali na la kihitoria kwa serikali yao kwa kushindwa kuchapisha kwa uwazi ushauri uliotolewa na wanasheria juu ya vigezo na masharti ya Uingereza kujiondoa katika umoja wa Ulaya.

Kura ya maoni inaelezwa kuwa na athari ndogo kwenye mjadala wa Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya huku mvutano wa wazi baina ya Bunge na Serikali ukionekana waziwazi kwa wabunge kumshambulia Waziri mkuu, Theresa May aliyetambulisha mpango wa Uingereza kujitoa.   

Wabunge 311 wameunga mkono karipio hilo la Bunge dhidi ya wabunge 293 na wamesema hiyo ni ishara ya wazi kwamba kwa mara ya kwanza serikali imelidharau Bunge.

Suala la usalama ni kipaumbele katika siku tano (5) nyingine za mjadala katika Bunge huku wabunge kadhaa wakitarajia kuwa na sauti moja ikiwa mpango wa Waziri Mkuu Thereza May utakwama wiki ijayo.

Mpango wa Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya ulipata baraka za Umoja huo lakini ni lazima uungwe mkono na Bunge la Uingereza, Disemba 11 watakapoamua ikiwa wakubaliane na mpango huo ama la!

Bunge
Maoni