Wachimbaji wadogo Tanga,Pwani na Moro watangaziwa neema

|
Waziri wa Madini, Anjela Kairuki akitoa maelekezo ya ujenzi wa Kituo cha Mafunzo na maarifa kinachojengwa Wilayani Handeni mkoani Tanga

Wachimbaji wadogo wa madini waliopo katika mikoa ya Tanga, Pwani na Morogoro wanatarajia kunufaika kupitia  mafunzo ya namna bora ya uchenjuaji, uchimbaji wa madini na utoaji mafunzo kwa biashara ya madini utakaotolewa na Kituo cha Mafunzo na Maarifa kinachojengwa wilayani Handeni mkoani Tanga.

Hayo yamebainika kufuatia ziara ya Waziri wa Madini, Anjela Kairuki anayetembelea wilayani Handeni kwaajili ya kujionea hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa kituo hicho  unaotekelezwa na  mkandarasi Suma Jkt Northern Zone ambapo ameagiza kikamilike kwa wakati na kikabidhiwe mikononi mwa Serikali  ifikapo Januari 15, mwakani.

Mradi huo ambao utagharimu zaidi ya Bilioni Moja mpaka kukamilika kwake tayari umeshaanza .

Madini
Maoni