Wafanyabiashara na DC washindwa kuelewana Mbeya

|
Wafanyabiashara wa mkoani Mbeya wakimsikiliza mkuu wa wilaya katika mkutano wa kujadiliana namna ya kupeana vitambulisho vilivyotolewa na TAMISEMI

Kikao kati ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika na madereva bodaboda kuhusiana na vitambulisho kimeshindwa kufikia mwafaka na kuvunjika baada ya kushindwa kuelewana.

Sintofahamu hiyo imetokana na Serikali hiyo ya wilaya kushindwa kuwafafanulia ikiwa wao wanalipa TRA, SUMATRA, Ushuru wa Jiji itakuwaje huku wakitakiwa kulipia  vitambulisho hivyo shilingi 20,000.

Kikao hicho kiliitishwa na mkuu wa wilaya hiyo kikiwa na lengo la kuwaelea madereva hao umuhimu wa vitambulisho hivyo na kuwataka madereva kwenda kwenye ofisi za watendaji wa kata kuvichukua kwa gharama ya shilingi 20,000.

Katika awamu ya pili Mkoa wa Mbeya umepewa vitambulisho 80,000 na Jiji la Mbeya pekee limepewa vitambulisho 45,000.

Biashara
Maoni