Wakala wa chakula waagizwa kubadili mfumo wa usafirishaji mahindi

|
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akizundua mtambo wa kusafishia mahindi uliotolewa na Shirika la Mpago wa Chakula Duniani (WFP).

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Nchini (NFRA) umeagizwa kubadili mfumo wa usafirishaji wa mahindi pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji ili Taasisi hiyo ijiendeshe kwa faida badala ya kupata hasara mara kwa mara.

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga ametoa maagizo hayo kwa NFRA Dodoma na kuwataka kuongeza kasi ya ununuzi wa mazao yote ya ziada ya wakulima kufikia tani 500,000 ambapo amezindua mtambo maalum wa kusafisha mahindi uliotolewa na Shirika la Mpago wa Chakula Duniani (WFP).

Waziri Hasunga amesema Wakala wa Taifa Hifadhi ya Chakula Nchini wanatakiwa kujenga maghala mazuri ya kutunzia nafaka.

Katika hotuba yake Waziri Hasunga aliwataka wakala hao kupunguza gharama za uendeshaji ili kuendesha taasisi hiyo kwa faida.

Katika hatua nyingine waziri Hasunga aliwasisiti Wakala wa Chakula Nchini kuhakikisha wananunua mazao ya ziada yaliyopo kwa wakulima.

Pamoja na mambo mengine Waziri Hasunga amewataka Wakala wa Taifa kuhifadhi Mahindi na kutumia vizuri mtambo huo na kuhakikisha wanachekecha mahindi hayo na kuyaweka katika ubora ili yaweze kuingia katika ushindani wa soko la kimataifa.

Chakula
Maoni