Walinzi mpakani mwa Marekani na Mexico walalamikia kuelemewa

|
Wahamiaji wanaosubiri kuingia Marekani wakivunja sheria kwa kuruka ukuta baada ya kuchoka kusubiri sana

Walinzi wa usalama katika mpaka wa Marekani na Mexico wamesema kumekuwa na ongezeko la idadi ya wahamiaji wanaoingia Califonia kinyume cha sheria tangu msafara wa wahamiaji kutoka Amerika ya Kati kuwasili katika mji wa Tijuana huko Mexico wiki mbili zilizopita.

Picha za video zimewaonesha wahamiaji wakiruka ukuta kutoka Tijuana kuingia Califonia baada ya kukata tamaa kutokana na urasimu katika utaratibu wa kisheria wa kuwapokea.

Marekani ilitangaza kuwa na uwezo wa kusajili wahamiaji 100 kwa siku, huku maelfu ya wahamiaji wakiendelea kusubiri mpakani.

Hata hivyo baadhi ya wahamiaji waliohojiwa wameonesha nia ya kuvumilia na kufuata sheria na kuomba vibali vya kazi.

Wengi wa wahamiaji wamekuwa barabarani kwa zaidi ya wiki saba sasa, tangu msafara wao ulipofika Tijuana kutoka Honduras.

Utawala
Maoni