Waliokufa kutokana na kimbunga Idai wafikia 417 nchini Msumbiji

|
Maeneo ambayo yameathirika na kimbunga Idai na kusababisha idadi kubwa ya wananchi kupoteza maisha yao

Idadi ya watu waliokufa kutokana na kimbunga cha Idai kilichosababisha mafuriko makubwa nchini Msumbiji imeongezeka maradufu kutoka watu 242 hadi 417, amesema waziri wa Ardhi na Mazingira wa Msumbiji, Celso Correia.

Idadi hiyo mpya inafanya idadi kamili ya vifo kwa nchi tatu za kusini mwa Afrika, Msumbiji, Malawi na Zimbabwe zilizoathiriwa na kimbunga hicho kufikia 700.

Vifo zaidi vinatarajiwa huku mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ukiripotiwa kutokea katika baadhi ya maeneo hali inayoongeza wasiwasi wa ongezeko la vifo.

Kimbunga Idai kimeua takribani watu 259 nchini Zimbabwe huku nchini Malawi vikiripotiwa vifo 56.

Hata hivyo Umoja wa Mataifa umesema unaweza kutambua madhara halisi pindi maji yaliyofunika baadhi ya maeneo yatakapopungua.

Maisha
Maoni