Wanafunzi dunia washinikiza dunia salama

|
Miongoni mwa wanafunzi nchini Australia walioandamana leo kupinga mabadiliko ya tabia nchi

Wanafunzi katika zaidi ya nchi 100 kote duniani leo Ijumaa wameyaacha madarasa yao ili kushiriki maandamano ya mitaani kuwashinikiza viongozi wa ulimwengu kuchukua hatua juu ya mabadiliko ya tabianchi.

Wanafunzi hao waliokuwa wamebeba mabango walionekana kutuma jumbe mbalimbali kwa viongozi wao huku wakionesha hasira za kutofanyia mzaha suala hilo na kusema hakuna sayari nyingine wanayoweza kuishi baada ya hii kutoweka na hivyo kutaka dunia salama kwa mustakabali wao.

Wanafunzi hao maelfu duniani waliacha vipindi madarasani kwa ajili ya siku ya leo ili kupaza sauti zao kupinga mabadiliko ya tabianchi.

Miongoni mwa nchi zilizopaza sauti kupitia wanafunzi hao ni India,Korea Kusini, Australia na Ufaransa.

Wanasayansi wanasema licha ya kelele nyingi na mikataba inayosainiwa jitihada zaidi na hatua madhubuti zinahitaji kuchukuliwa kwa lengo la kuondokana na joto kali linaloikumba dunia.

Ikumbukwe kuwa, katika makubaliano ya Paris climate ya mwaka 2017 takribani nchi 200 zilikubaliana kupunguza kiwango cha joto duniani kufikia cha "chini ya"  Sentigredi 2.0  hadi sentigredi 1.5.

Mazingira
Maoni