Wanafunzi Kwechigwe wapata afueni ya kukaa madarasani sasa

|
Wafadhili wa Tanza Care wakishuhudia ukaaji darasani wanafunzi wa shule hiyo walisaidia ujenzi wa madarasa

Wanafunzi wa Shula ya Msingi Kwechigwe wilayani Handeni mkoani Tanga, wameondokana na adha ya kusomea chini ya miti baada ya kujengewa madarasa matano.

Kati ya madarasa hayo matano, mawili yamejengwa na shirika lisilo la kiserikali la Tanzana Care lenye makazi yake nchini Marekani na matatu yamejengwa na Serikali.

Awali wanafunzi hao walikuwa wakisoma chini ya mti jambo ambalo lilikuwa linasababisha wasifanye vizuri kwenye masomo yao.

Kaimu Mkuu wa Shule ya Kwachigwe,  Seleman Haji amesema kuwa tangu shule hiyo ipate madarasa wanafunzi wamekuwa na ufaulu mzuri ukilinganisha na kipindi cha nyuma.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tanza Care, Kerry Gaines amesema kuwa wataendelea kusaidia katika shule mbalimbali nchini lengo likiwa ni kuona wanafunzi wakitanzania wanafaulu vizuri masomo yao.

Elimu
Maoni