Wanaoishi na VVU walalamikia Serikali kutowapa ushirikiano

|
Vidonge vya kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi kwa waathirika

Inadaiwa kuwa Serikali na vikundi vya wanaoishi na VVU kuanzia ngazi za chini hawana uhusiano mzuri na hivyo kushindwa kufikia malengo yaliyowekwa katika mapambano dhidi ya Ukimwi.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa kitengo cha taarifa (NACOPHA), Daud Kweba alipokuwa akizungumza na Azam news mkoani songwe walipokuwa wakitembelea vikundi hivyo katika Wilaya ya Mbozi.

Katika ziara hiyo iliyolenga kutembelea vikundi hivyo, pia walipata nafasi ya kujifunza mbinu za namna watu hao wanaoishi na VVU sanjari na  kuendesha vikundi.

Hata hivyo Mratibu huyo wa NACOPHA aliridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Kikundi cha Jitegemee kilichopo katika Kijiji cha Ichesa wilayani Mbozi mkoani Songwe kutokana na kuwa cha mfano kwa kuwa na mafanikio na kuishi kwa kujitegemea.

Naye Katibu wa Kikundi hicho cha Jitegemee, Sophia Nyungu alimwelezea mratibu huyo mafanikio ambayo wameyapata tangu kuanzishwa kwa kikundi hicho na kutoa rai kwa wengine kujitokeza na kupima afya zao ili waweze kujitambua mapema.

Kikundi hicho cha jitegemee ni moja kati ya vikundi 80 vya wa VVU wilayani Mbozi ukiachilia mbali shughuli wazifanyazo pia uhamasisha wengine waweze kupima maambukizi ya Ukimwi.

Afya
Maoni