Wanawake wang'ara tuzo za 61 za Grammy Marekani

|
Mke wa rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama akiwa katika picha ya pamoja na wanamuziki wanawake wanavuma nchini Marekani wakati wa tuzo za Grammy

Wanamuziki Dua Lipa won na mwenzake Kacey Musgraves wamejishindia tuzo za muziki wa 61 za Grammy kwa upande wa wanawake, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, Jumatatu huko Marekani.

Dua Lipa amechukua tuzo hiyo kama mwanamuziki mpya katika tuzo hizo huku Kacey akichukua tuoz ya albamu bora ya mwaka na ya kwanza kwa upande wa wanawake.

Musgraves mbali na kushinda tuzo ya albamu bora, pia ameshinda jumla ya tuzo Nne katika saa za dhahabu.

Akipokea tuzo hizo Musgraves amesema ameitunuku tuzo hiyo kwa "mume wake kipenzi" ambaye walipenda wakati akirekodi albamu hiyo.

Kwa upande wake Dua amesema alikuwa na "hofu na furaha "  wakati akipokea tuzo hiyo katika usiku huo wa tuzo bora na kubwa kabisa kupokea.

Mwanamuziki huyo mwenye miaka 23 alitoa heshima pia kwa wanawake wasanii ambao wengi wao waliokwishapitia ambapo alisema: " Nafikiri kwa mwaka huu tumeongezeka."

Kauli hiyo imepokelewa kama kuunga mkono matamshi ya Rais wa tuzo hizo za Grammy, Neil Portnow, ambaye mwaka jana alijaribu kufafanua kuhusu ukosoaji wa kuwa tuzo hizo zimekosa washindi wanawake ambaye alisema, wanawake wanahitaji  " kujiongeza kwa ajili ya kuchukuliwa kwa uzito.

Wakati huo huo, mke Rais mstaafu wa Marekani, Michelle Obama alijitokeza katika mkusanyiko huo kwa kushtukiza akiwa amefuatana na wanamuziki nyota  akiwemo Lady Gaga, Jada Pinkett-Smith, Jennifer Lopez na  Alicia Keys na kutoa hotuba iliyobeba ujumbe murua kwa wahudhuriaji wa sherehe za tuzo hizo.

"Haijalishi tunapenda nini, uwe unapenda muziki wa country au rap au rock, muziki hutusaidia kuunganisha hisia zetu wenyewe , uchungu wetu, heshima yetu, matumaini yetu na hata furaha  zetu," ilinukuliwa sehemu ya hotuba yake hiyo ambapo alisema. "Muziki unaturuhusu kusikiliza wenyewe kwa wenyewe, na kualikana kila mmoja wetu." 

Maisha
Maoni