Wanawake watakaozaa watoto wanne Hungary kusamehewa kodi

|
Wanawake watakaozaa watoto wanne kusamehemewa kodi

Wanawake wenye watoto wanne au zaidi nchini Hungari wanatarajiwa kupatiwa msamaha wa kodi kwa maisha yao yote.

Akizungumzia mpango huo unatarajiwa kuanza hivi karibuni, Waziri mkuu wa nchi hiyo, Viktor Orban amesema unalenga kuhamasisha wanawake kuzaa watoto zaidi ili kuongeza idadi.

Amesema njia hiyo ni moja ya mkakati wa kuiwezesha Hungari baadaye kuwa na uwezo wa kujitegemea wenyewe bila wahamiaji.

Mara kwa mara wazawa wa Taifa hilo wenye mrengo wa kulia wamekuwa wakipinga uingiaji wa wahamiaji hususan Waislamu.

Idadi ya watu nchini Hungari hushuka kwa jumla ya watu 32,000 kila mwaka, huku wanawake wakiwa na watoto wachache zaidi ikilinganishwa na wastani kwa wanachama wengine wa nchi za Ulaya.

Katika mkakati huo, hatua nyingine zitakazochukuliwa ni kwa wanandoa wachanga watakuwa wakipatiwa ofa ya mkopo bila riba  iwapo watakopa dola za kimarekani 36,000 na utasitishwa kulipwa punde watakapofanikiwa kupata watoto watatu.

Akizungumzia sababu ya kupungua kwa kiwango cha kuzaa, Orban amesema, kwa upande wa magharibi, jibu ni wahamiaji : " Kila anapokosekana mtoto, kuna anayekuja na hivyo kuifanya idadi ya watu kuwa sawa.

"WaHungari watu wanafikiri tofauti," amesema. "Hatuhitaji idadi ya watu. Tunachotaka ni watoto wa KiHungari."

Maisha
Maoni