Wanawake wauza chaza Unguja walilia soko la uhakika

|
Chakula aina ya chaza wanaopatikana baharini wakiwa wameshaandaliwa tayari kwa kuliwa

Wanawake wanaojishughulisha na uchokoaji na uuzaji Chaza waliopo Kikungwi Mkoa wa Kusini Unguja wamesema kukosekana kwa soko la uhakika kunarejesha nyuma harakati zao za kujikwamua kiuchumi.

Wakizungumza na Azam News wamesema wanatumia sehemu za pembezoni mwa barabara kuuza kitoweo hicho hali inayoweza kuhatarisha maisha yao.

Chaza, ni miongoni mwa vitoweo maarufu visiwani Zanzibar, ingawa upatikanaji wake unahitaji ujasiri.

Wanawake hao ambao wengi wao huishi maeneo ya pwani hujishuhulisha na kazi hiyo kwa lengo la kujiongezea kipato katika familia zao.

Shughuli ya utafutaji chaza inafanyika katika Kisiwa cha Ukanga kilichopo nje kidogo ya Kisiwa cha Unguja,

Baada ya shughuli hiyo chaza hupikwa ili wawe tayari kwa ajili ya kuuzwa.

Wakizungumza na Azam TV, wanawake hao wamesema licha ya kazi hiyo kuwapatia kipato lakini wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wake kutoka na kwamba wanatumia boti za watu na kuiomba serikali iwasaidia kupatikana kwa boti watakayokuwa wakiitumia kutafutia kitoweo hicho sambamba na kuwatafutia soko.

Mbali ya wanawake hao kufanya shughuli hiyo wapo pia baadhi ya wanaume wanaozamia kwaajili ya kuvua kome na jamii nyingine ya vitoweo vya baharini ambao wanaziomba mamlaka husika kuwatafutia soko la uhakika la nje ya nchi.

Chakula
Maoni