Wapendanao wapatiwa shilingi 346,000 kutoka kwa msamaria mwema

|
Timotheo Richard (30) akiwa amempakiza mkewe Salome Msombe (31) baada ya kupokea msaada wa fedha kutoka kwa msamaria mwema

Upendo wa kweli haubagui ndivyo unavyoweza kusema kupitia mapenzi ya Timotheo na Salome.

Baada ya Azam TV kurusha taarifa yao na kuenea hadi nje ya nchi hatimaye wadau mbalimbali wamejitokeza na kuanza kuwasaidia kifedha.

Miongoni mwa waliojitoa ni raia wa DR Congo anayeishi nchini Uingereza Maria Lee Lion De Tong aliyewachangia shilingi 346,000 ambazo zilitumwa kwa njia ya Western Union.

Wapendanao hawa wameishukuru Azam TV kwa kutangaza hadharani kuhusu upendo wao huo ambao umekuwa gumzo kwa watu wengi kila wanapowaona.

Maisha
Maoni