Wasafirishaji viumbehai wamwangukia Rais Magufuli

|
Viumbe hai ambavyo vimezuiwa kusafirishwa nje ya nchi

Chama cha Wasafirishaji wa Viumbepori hai nje ya nchi wamemuomba Rais John Magufuli kuingilia kati zuio walilowekewa na wizara husika kutosafirisha viumbe hivyo kwa muda wa miaka mitatu.

Wamebainisha hayo leo walipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,  ikiwa ni miaka mitatu sasa tangu kuwekwa kwa zuio hilo na hakuna dalili zozote za kufunguliwa licha ya kuwa wakifuatilia Wizara ya Maliasili na Utalii mara kwa mara .

Wasafirishaji hao wamesema, wanaimani Rais Magufuli atalichukulia suala lao hilo kwa umakini na kuongeza kuwa licha ya kusimimashwa kufanya biashara hiyo kwa miaka mitatu, lakini hata hivyo wamekuwa wakilipia leseni  zao na kwa mwaka huu wameshalipa takribani milioni 17.

Wafanyabiashara hao ambao jumla yao ni 454 wenye leseni wamemuomba Rais Magufuli na wizara husika kuwasaidia kulitatua suala hilo kutokana na ukweli kwamba kazi hiyo ndiyo inayowawezesha kuendesha maisha yao na familia zao sanjari na kuliongezea pato la Taifa.

Biashara
Maoni