Washtakiwa wa kesi ya utoroshaji dhahabu wafikishwa kortini tena

|
Watuhumiwa wa utoroshaji wa dhahabu wakiwa mahakamani mkoani Mwanza

Kesi ya utoroshaji dhahabu inayowakabili washtakiwa 12 wakiwemo askari polisi wanane imetajwa tena leo, Jumatano jijini Mwanza ambapo kumekuwepo na taratibu za kisheria za upande wa mashtaka kubadilisha hati ya mashtaka hali iliyosababisha keshi hiyo kuchelewa kutajwa.

Kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba tatu ya mwaka 2019 inawakabili washtakiwa  hao 12 kwa kosa la utoroshaji wa dhahabu Kilogramu 319 yenye thamani shilingi bilioni 27 na inasikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Mwanza.

Wanaotuhumiwa katika kesi hiyo ni wafanyabiashara Sajid Hassan na Hassan Hassan wenye asili ya kiasia pamoja na Kisabo Mkinda na Emanuel Ntemi  huku wengine ni waliokuwa askari polisi akiwemo  aliyekuwa Mkuu Operesheni, Moris Okinda, Daniel Kasara, Mtete Misana , Japheti Lukiko, Maingu Sorra, Alex Nkali, Timoth Nzumbi na David Ngelela.

Mahakamani
Maoni