Washtakiwa wa mauaji wafikishwa mahakamani Njombe

|
Washtakiwa wa mauaji na mtoto moja wakiwa mahakamani mkoani Njombe

Washtakiwa wa tatu wa kesi ya mauaji ya mtoto, Rachel Malekela aliyeuwawa mwezi Februari katika Kijiji cha Matembwe, Tarafa ya Lupembe wilayani Njombe wamefikishwa kwa mara ya tatu  katika Mahakama ya Hakimu mkazi Wilaya ya Njombe.

Washtakiwa hao ambao ni Mariana Malekela, Edwin Malekela pamoja na Kalitus Ndiungwa wanashtakiwa kwa kosa la mauaji ya mwanafunzi, Rachel Malekela aliyekuwa na umri wa miaka Saba Mkazi wa Kitongoji cha Lung'angale, Tarafa ya Lupembe, wilayani Njombe ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Matembwe ambaye aliuawa Februari Mosi mwaka huu na mwili wake kukutwa  umetupwa kichakanj jirani na makazi ya nyumba yao.

Shauri hilo lililosomwa na mwendesha mashtaka wa serikali, Nura Manja mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe, James Mhanusi limeahirishwa  kutokana na upelelezi kutokamilika na inatarajiwa kusomwa tena Aprili Mosi mwaka huu.

Mahakamani
Maoni