"Watakaoshindwa kuwapeleka watoto shule kukiona Kibaha"

|
Wananchi wa kijiji cha Kwala na Mwembengozi wakimsikiliza mkuu wao wa Wilaya ya Kibaha, Asumpta Mshana

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshana ameagiza watendaji wote wa Kijiji cha Kwala na Mwembengozi kuhakikisha watoto wote wa wafugaji jamii ya Kimasai na Wamang'ati wanaenda shule badala ya kufanya kazi ya kuchunga ng'ombe.

Mkuu huyo wa wilaya amesema, haoni sababu ya watoto hao kukosa elimu wakati Rais wa nchi ametoa fedha nyingi ajili ya Watanzania kupata Elimu bure .

Aidha amewaonya wafugaji watoto watakao kutwa kuanzia Jumatatu wanachunga, mzazi wa mtoto husika atachukuliwa hatua kali na kufikishwa mahakamani.

Hayo amezungumza alipotembelea Kijiji Cha Kwala ikiwa ni ziara ya kumaliza mgogoro baina ya wakulima na wafugaji ambao ulidumu kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita na kufanikiwa kuumaliza leo Machi 14.

Elimu
Maoni