Watanzania kushuhudia tamasha la sanaa ya mapishi ya Ufaransa

|
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tamasha la Mapishi ya vyakula vizuri vya Ufaransa, jijini Dar es Salaam

Jumla ya wapishi 30 wa Hoteli ya Hyatt Machi 21 wanatarajia kunufaika na mafunzo ya mapishi ya vyakula vyenye ladha ya kifaransa yatakayoenda sambamba na hafla ya kusheherekea sanaa ya mapishi ya chakula kizuri ( Gastronomy Cuisine).

Wapishi hao watapatiwa mafunzo hayo ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufanyika nchini, lengo likiwa ni kuhakikisha kazi ya upishi inakuwa sehemu ya kukuza uchumi na kuongeza ajira.

Akizungumzia tukio hilo maarufu nchini Ufaransa ambalo kwa mwaka huu litaadhimishwa Machi 23, Balozi wa Ufaransa nchini, Frederic Clavier amesema jumla ya wapishi takribani 5000 watashiriki sanaa hiyo ya mapishi ya kupika chakula kizuri ( Gastronomy Cuisine).

Clavier amesema, sanaa hiyo kwa sasa imetambuliwa rasmi na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu (UNESCO) kutokana na kuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi, kuongeza ajira na fursa mbalimbali za kimaendeleo.

Sanaa hiyo ya mapishi nchini, itahusisha wapishi hao wa ndani ambao watapika chakula hicho chenye ladha ya kifaransa kwa kutumia bidhaa na viungo vya ndani kwa lengo la kuhakikisha watanzania watakaoshiriki usiku huo wa kula chakula kitamu cha kifaransa wanafurahia ladha ya vyakula walivyovizoea.

Tamasha la sanaa ya mapishi ya vyakula vitamu lilianza tangu mwaka 2015 huko nchini ufaransa na limekuwa likipata umaarufu na hadi sasa limekuwa likisheherekewa sehemu mbalimbali duniani huku likihusisha wapisha na watu mbalimbali.  

Chakula
Maoni