Watu 8 wanaosadikiwa kuwa majambazi wauawa Mwanza

|
Watu 8 wanaosadikiwa kuwa majambazi wauawa Mwanza

Watu nane wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa usiku wa kuamkia leo katika kisiwa cha Ukerewe jijini Mwanza kwenye majibizano ya risasi na Jeshi la polisi yaliyodumu kwa takribani saa tatu.

Tukio hili limetokea leo 26/01/2019 majira ya saa moja hadi saa tatu usiku katika daraja linalotenganisha vijiji vya Buhima na Ilaga.

“Tulipata taarifa za kiintelijensia kwamba Wilayani Ukerewe kumeingia majambazi wapatao kumi wenye silaha za moto wakiwa na nia ya kupora fedha na vitu mbalimbali kwenye maduka na katika makazi ya watu mjini Nansio,” alisema Kamanda Mkoa wa Mwanza, Janathan Shana.

katika tukio hilo polisi ilifanikiwa kukamata silaha moja aina ya AK47 isiyo na namba, na short gun moja iliyotengezwe kienyeji na risasi 15 za AK47, Magazine mbili, Risasi 15 za AK47, Maganda 23 ya silaha aina ya AK47, panga moja, nondo moja na simu sita.

 

Aidha katika tukio hilo hakuna askari yeyote aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa.

“Miili ya majambazi hao imehifadhiwa hospitali ya Wilaya ya Ukerewe kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi, pindi uchunguzi ukikamilika itakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi,” alisema Shana.

 

Tukio
Maoni