Waumini wa Kiislamu waanza kutekeleza ibada ya mfungo

|
Ramadhan Kareem

Kufuatia kuandama kwa mwezi kesho Waumini wa Dini ya Kiislam wanaanza kutekeleza ibada ya mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni moja kati ya nguzo tano za Uislam ambapo watafunga kwa siku ishirini na tisa au thelathini.

Ibada hiyo inaanza kutekelezwa kipindi hiki hali ya upatikanaji wa futari kwenye maeneo mengi ikielezwa ni nzuri, huku bei nazo zikiwa za kawaida ambazo waumini wanaweza kuzimudu.

Hiki ni kipindi cha waumini wa Kiislam kuchuma thabawu kwa kila jema ambalo wanalitenda malipo yake huwa maradufu ukilinganisha na miezi mingine kumi na moja.

Wakati ambapo futari ndiyo chakula maarufu zaidi ambapo wafanyabiashara na wanunuzi wanaeleza hali halisi ya upatikanaje wake pamoja na bei zilivyo.

Utawala
Maoni