Wauza madafu Zanzibar walilia soko kushuka

|
Biashara ya madafu

Wafanyabiashara wa Madafu visiwani Zanzibar wamesema hali ya soko la bidhaa hiyo kwasasa imeshuka kutokana na upatikanaji mdogo wa madafu unaosababishwa na kuwekwa kwa minazi maalumu ya madafu.

 

Wakizungumza na Azam News wafanyabiashara hao wamesema serikali imelazimika kuweka minazi maalumu ya madafu ili kuzuia hali ya upungufu wa nazi visiwani Zanzibar. 

Dafu, ni miongoni mwa vivywaji pedwa na vya asili visiwani Zanzibar, licha ya kupendwa sana kinywaji hicho lakini pia watu hukitumia kama dawa.

 

Kwa miaka ya nyuma kidogo dafu lilionekana kukosa thamani kutokana na jamii kutokua na mwamko wa kutumia kinywaji hicho tofauti na miaka ya hivi karibuni thamani yake imeongezeka kutoka shilingi 500 hadi 1000 kutokana na ugumu wa upatikanaji wake.

  

Mbali na kuuza biashara hiyo wafanyabiashara hao wamesema wanazo changamoto kadha zinazowakabili katika uuzaji wa bidhaa hiyo.

 

Kwa upande wa watumiaji wa kinywaji hicho wameishauri jamii kutumia zaidi vinywaji vya asili ili kuimarisha afya zao na kuepukana na magonjwa yanayosababishwa na ulaji mbaya.

Biashara
Maoni