Waziri Jafo aiagiza UDART kuongeza mabasi kumi

|
Mabasi ya mwendokasi ambayo sasa Serikali imeagiza yaongezwe kwa njia ya Kimara

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amemuagiza Mtendaji mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka kuongeza mabasi Kumi ya njia za pembeni (Feeder Roads) wakati wa asubuhi na jioni kutoka Kimara kuelekea Kivukoni na Gerezani ili kupunguza tatizo lililopo la upungufu wa mabasi hayo jijini Dar es Salaam huku akitaka mabasi mabovu yatengenezwe haraka.

Lakini pia Waziri Jafo amemtaka Mtendaji mkuu wa DART, kuwasilisha majina ya watendaji ambao wanamkwamisha huku akimsisitizia kuwasiliana na wataalam wa TEHAMA na Wizara ya Fedha ili kuondokana na mfumo wa malipo kwa kutumia risiti na badala yake watumie kadi.

Suala la vyombo vingine vya moto kupita katika barabara ya mwendo wa haraka nalo akaligusia na kulitaka Jeshi Polisi kwa kushirikiana  na askari wa usalama barabarani  kuhakikisha hakuna anayetumia barabara hiyo maalumu ya mabasi ya mwendo wa haraka kwa sababu matumizi hayo ni chanzo kimojawapo cha uharibifu wa mabasi hayo.

Usafiri
Maoni