Waziri Mbarawa awapa 'makavu' mamlaka za maji nchini

|
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na watumishi wa mamlaka ya maji Mbeya

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amesema kwa sasa wizara yake haina mpango wa kupeleka fedha kwenye miradi inayosimamiwa na mamalaka za maji ambayo inaweza kutekelezwa na mamlaka hizo kupitia mapato ya ndani.

Badala yake Waziri Makame ameeleza kuwa wizara yake itakuwa na jukumu kubwa la kusimamia miradi inayohitaji fedha nyingi ambazo haiwezi kutekelezwa na Mamlaka hizo.

Waziri Mbarawa ametoa kauli hiyo alipozungumza na watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira MBEYA UWSA mkoani Mbeya.

Hata hivyo Waziri Mbarawa ameshangazwa na makusanyo kushuka kutoka shilingi bilioni 1.1 kwa mwezi Januari hadi shilingi milioni 900 na kuihoji bodi inayosimamia mamlaka hiyo kushindwa kusimamia vyema majukumu yake.

Maji
Maoni