Waziri Uingereza adai mashambulizi dhidi ya Syria ni sahihi

|
Boris Johnson, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Boris Johnson amesema hatua zilizochukuliwa na Ufaransa, Uingereza na Marekani dhidi ya Serikali ya Bashar Al Assad ni sahihi na zinalenga kudhibiti uwezo wa silaha za kemikali wa serikali hiyo.

Waziri Johnson ameyasema hayo akiwa nchini Luxembourg ambako mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana kujadili hali ya Syria.

Amesema mashambulizi yanayofanyika nchini Syria hayana lengo la kuomuondoa madarakani Rais Assad au kubadili wimbi na mwelekeo wa vita.

“Ukiangalia kilichotokea AprilI 7 huko Douma, unaweza kuona kuwa hatua iliyochukuliwa na Ufaransa, Uingereza na Marekani kwa kuanzisha mashambulizi dhi ya Rais Assad wa Syria na uwezo wake wa silaha za kemikali  ulikuwa sahihi kufanyika kwa ujumla wake, - sahihi kwa Uingereza na sahihi kwa dunia.

“Na ninaona fahari kwa sababu za wazi juu ya uugwaji mkono tunaopata kutoka jumuiya ya kimataifa, na ni muhimu kusisitiza kuwa hatua hii haina lengo la kubadilisha uongozi nchini Syria au kuondoa madarakani Bashar al-Assad.“ alisema Boris.

Utawala
Maoni