Waziri wa usalama wa ndani Marekani aachia ngazi

|
Waziri wa Usalama wa ndani wa Marekanii, Kirstjen Nielsen

Waziri wa Usalama wa ndani wa Marekanii, Kirstjen Nielsen, ambaye pia alitekeleza baadhi ya sera zilizokuwa na utata za Rais Donald Trump amejiuzulu.

Mwanamama Nielsen katika taarifa yake ya kujiuzulu ameiita nafasi hiyo aliyopewa kuwa,  "ni heshima kubwa katika maisha yake" kufanyia kazi idara hiyo.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Rais Trump ameandika kuwa, nafasi ya mwanamama huyo itazibwa kwa muda na Kamishna wa Ulinzi wa Mipaka na ushuru, Kevin McAleenan.

Nielsen atakumbukwa kwa kutekeleza bila kusita pendekezo la ujenzi wa ukuta mpakani mwa Marekani na Mexico pamoja na sera ya kutenganisha familia za wahamiaji nchini Marekani.

Katika barua yake ya kujiuzulu, waziri huyo hajatoa sababu zaidi za kwanini amefikia uamua huo ingawa amesisitiza kuwa “huu ni muda muafaka wa yeye kukaa pembeni" na kuongeza kuwa Marekani kwa sasa "iko salama leo zaidi ya wakati alipojiunga na utawala wa Trump".

Utawala
Maoni