WHO: Chukula kisicho salama huua idadi kubwa ya Waafrika

|
Chakula kisicho salama huua idadi kubwa ya waafrika

Takribani watu milioni 600 duniani wametajwa kuugua kila mwaka kutokana na kula chakula kisicho salama na kati ya hao 420,000 hupoteza maisha kutokana na tatizo hilo huku idadi kubwa ikitajwa kuwa iko zaidi barani Afrika ambapo zaidi ya watu milioni 91 wanakadiriwa kuugua na watu 137,000 hufariki kila mwaka kutokana na kula chakula kisicho salama.

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), zilizotolewa mwaka 2015 ambapo magonjwa ya kuhara yametajwa kuchangia kwa asilimia 70 ya magonjwa yote yatokanayo na chakula barani Afrika na hivyo kubainisha uwepo wa tatizo kubwa la uchafuzi wa vimelea vya maradhi katika chakula.

Hayo yameelezwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita, Simon Ndario wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watumishi wa Sekta ya Afya kwaajili ya utekekezaji wa Mpango wa Ufuatiliaji wa Magonjwa yatokanayo na Chakula.

Mafunzo hayo yaliandaliwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).

Chakula
Maoni