Yanga yaanza kwa kutoa dozi Mapinduzi Cup

|
Ni baada ya goli la Yanga kufungwa.

Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC wameanza vizuri michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar kwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya vinara wa Ligi ya Zanzibar KVZ katika mchezo wa kundi B uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan.

Licha ya kukabiliwa na upinzani mkubwa kwenye mchezo huo, Yanga iliyoundwa na wachezaji zaidi ya saba wa kikosi cha vijana, ilipata bao lake pekee la ushindi dakika ya 76 ya mchezo kupitia kwa Shaban Mohamed akiitumia vema pasi kutoka kwa Matheo Anthony.  

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuongoza kundi lake ikiwa na pointi 3, mbele ya Azam wenye alama 1, Jamhuri alama 1, Malindi alama 1 na KVZ alama 1.  

Leo Januari 4 kutakuwa na michezo miwili ambapo saa 10:15 ni Jamhuri dhidi ya Malindi kutoka Kundi B, na saa 2:15 usiku ni mabingwa wa Tanzania Bara Simba dhidi ya Chipukizi.

Kombe la Mapinduzi
Maoni