Yondan avuliwa unahodha Yanga kwa utovu wa nidhamu

|
Ibrahim Ajibu amechaguliwa kuwa Nahodha mpya wa Yanga.

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amemvua kitambaa cha unahodha beki Kelvin Yondani na kumteua Ibrahim Ajibu kuwa nahodha mpya wa kikosi cha timu hiyo.

Zahera amesema amechukua uamuzi huo baada ya Kelvin kuonesha utovu wa nidhamu kwa kuchelewa kuripoti mazoezini baada ya siku tano za mapumziko alizowapa wachezaji wote kumalizika.

Kikosi kikuu cha Yanga SC kilichobaki jijini Dar kimeanza rasmi mazoezi leo baada ya mapumziko ya mwaka mpya na kuhudhuriwa na wachezaji wote ambao hawajaenda na timu Zanzibar huku nahodha mkuu wa kikosi hicho Kelvin Yondani akishindwa kuhudhuria bila taarifa yoyote.

"…Kuanzia leo Ajibu ndiyo atakuwa nahodha mkuu wa timu badala ya Yondan ambaye ameonesha utovu wa nidhamu kama kiongozi kushindwa kuhudhuria mazoezi bila kutoa taarifa kwangu au kwa wenzake," amesema Zahera.

Soka Tanzania
Maoni