Zitto ayataka matawi ya ACT Wazalendo kuorodhesha wanachama wao
|
Bendera ya ACT Wazalendo
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amewataka viongozi wa matawi kuorodhesha majina ya wanachama wao katika matawi waliyopo na kuwatambua huko huko ili kuepusha vurugu zisizo za lazima.
Kauli hiyo ameitoa katika ofisi za makao makuu ya chama hicho iliyopo Kijitonyama Dar es Salaam mara baada ya kuzuiwa na Jeshi la Polisi kufanya mkutano huo ambao walipanga kuufanya katika Ukumbi wa PR Stadium Temeke kupokea wanachama wapya 12,600.
Mkutano huo wa kupokea wanachama ulihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali akiwemo aliyekuwa makamu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi wengine ambapo wamepokea kadi zaidi ya 900.