Azam FC wavunja ratiba ya kambi ya Uganda

|
Kikosi cha AZAM FC

Uongozi wa klabu ya Azam FC jana umetangaza kuvunja ratiba ya kuweka kambi jijini Kampala Uganda kufuatia ujio wa michuano ya Kagame inayotarajia kuanza Juni 28 nchini.

Awali Azam walipanga kuisafirisha timu hiyo kwenda Uganda ikiwa ni mapema baada ya wachezaji wake kumaliza mapumziko waliyopewa ambapo yalipaswa kumalizika mwezi Julai.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Habari, Jaffer Maganga, wameamua kusitisha safari hiyo na badala yake wachezaji watakaporejea kutoka likizo wataanza kambi maalum ya kujiandaa na mashindano ya KAGAME.

"Tumeahirisha kuweka kambi Uganda kutokana na mashindano ya KAGAME, inabidi tuyape uzito ili tuweze tena kulitetea taji hilo," alisema Maganga.

Kutokana na ujio wa mashindano hayo, likizo ya wachezaji kurejea kambini mwezi Julai itabidi sasa isitishwe na badala yake watarejea mapema mwezi huu kwa ajili ya kuanza maandalizi.

VPL
Maoni