Brazil ndiyo timu yenye mafanikio zaidi - Kocha Tite amjibu Trump

|
Tite ameonesha ishara ya vidole vitano ikiwa ni jibu kwa Trump kuwa Brazil ndiyo timu yenye mafanikio zaidi duniani ikiwa imetwaa mara nao kombe la dunia.

Kocha wa Mkuu wa timu ya Taifa ya Brazil, Adenor Leonardo Bacchi maarufu kama Tite, amemjibu Rais wa Marekani Donald Trump kuwa Brazil ndiyo timu yenye mafanikio zaidi duniani kwa kutwaa kombe la dunia mara tano.

Majibu hayo ya Tite yamekuja siku chache baada Donald Trump kuidhihaki Brazil kuwa ina matatizo kiasi cha kutolewa kwenye robo fainali ya kombe la dunia na timu ya Ubegiji.

Trump alitoa kauli hiyo wakati akimpokea Rais FIFA Giann Infatino alipozulu Marekeni kutambulisha kombe la dunia litakalofanyika Marekani mwaka 2026.

Kauli hiyo imeonekana kumkera kocha Tite ambaye leo kwenye mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mechi ya kirafiki dhidi ya El Salvador, ameonesha ishara ya vidole vitano ikiwa ni jibu kwa Trump kuwa Brazil ndiyo timu yenye mafanikio zaidi duniani ikiwa imetwaa mara nao kombe la dunia.

Kombe la dunia
Maoni